Popular Posts

Friday, September 16, 2011

Kisa na Mkasa, Bongo Darisalama...

WALIMU wa MAZOEZI: KERO KATIKA MAHUSIANO!

Hapa jiran kuna Gym centre ambayo imekua ikihudhuriwa na wateja mara kwa mara nyakati za jioni (baada ya muda wa kazi kwa siku za kuanzia j3-ijumaa) na zaid siku za wikiend, kimsingi gym hii ipo ktk mazingira mazuri then huduma yake si haba, wafanyakazi wake ni wakarimu pia imesheheni walimu wazuri wenye kujua nin walifanyalo pindi wawahudumiapo wateja wao.

Kumekuwapo na tetesi kuwa mmoja wa walimu hao amekuwa akijihusisha/mahusiano ya kimapenzi na wateja wa kike mara kwa mara na tofauti muda tu wanapojiunga na kituo hicho, kwa kuwa wengi ya wateja wajao hapa wametokea/wapo safi kiuchumi hii imemfanya mwalimu huyu kuchukulia mahusiano haya km kitega uchumi, amekuwa akitembea na wake wa watu na kutumia vitu vyao km vile magari pasipo aibu wala uwoga wowote!

Kama waswahili wasemavyo siku ya mwizi ni arobaini, kumbuka hakuna siri ktk mapenzi, waswahili wamemfikishia bwana juu ya matendo ya mkewe na huyo mwalimu wa mazoezi, wamempa ratiba na mchakato mzima ile mwanzo mwisho, mke kama kawaida kaaga anaenda zoezi, mume pasipo onyesha mshituko wala wasiwasi kamkubalia, kaenda gym. Mke katangulia, baada ya muda bwana kamfuata kwa nyuma, kafika gym hamwoni pale pa siku zote, kwa kuwa si mgeni kaingia vyumba vya ndani vya kuchangea nguo napo kamkosa, kaamua kwenda bafuni, kahamaki kumkuta mke na mwalimu wa mazoezi wakifanya mambo, bwana kumbuka kajiandaa vya kutosha, kakasirika kawatoa nje km walivyo zaliwa, kawapakia kwenye gari kawapeleka kituoni. 
 
Huku nyuma kaacha gumzo. KILICHONIFANYA HASWA NILETE thread hii humu tofauti na kutoa habari ni pamoja na kutaka kuwaonyesha ni kwa kiasi gani hawa walimu wa mazoezi walivyokua mwiba katika mahusiano ya mapendanao, sijui ni kwa nini haswa bt hawa watu ni hatari, nadhani kuna kilasababu ya kuwakemea na kuchunga wapenzi zetu.K WA WALE mnaofahamu na mlio na ukaribu na hawa watu JE MWAWEZA KUTUGUSIA MBINU WATUMIAZO WATU HAWA KUDAKA WAKE/WACHUMBA/WAPENZI AU DADA ZA WATU? Nijuavyo mimi ni kuwa hawa WALIMU WA MAZOEZI NI JANGA LA KUEPUKA KATIKA MAHUSIANO, NI HATARI SANA, TUWATAFUTIE DAWA!
 
Habari kwa hisani ya JAMIIFORUM.

No comments: