Popular Posts

Friday, September 21, 2012

2nite @ Rudy's Farm...


The sexy & unique Bar at Rudy's 

farm, made of brick work burned 

RED, reclaimed dhow wood and 

recycled metal.... 

Twist the yard - with deejay 

handsolo on the mix - tonight!

Njooni WOTE!

Thursday, September 20, 2012

Matukio katika picha...

Moja kati ya bendi changa na zinazochipukia... ikiwa kazini!
 M
Juu na chini, need me say more?

Wednesday, September 12, 2012

Today's joke...


Jamaa alienda kuposa kwa mzee mmoja. 
Mzee:Umekuja  kuposa huku  unatafuna bigji!? 
Jamaa:Natoa harufu ya sigara. 
Mzee:Yani unavuta sigara!? 
Jamaa:Vile nikitoka kilabu kulewa tu huwa napenda kutumia sigara. 
Mzee:Unalewa!? 
Jamaa:Nilianza kulewa nilipokuwa jela. 
Mzee:Yaani na kufungwa pia!? 
Jamaa:Ah niliua mtu. 
Mzee:/uh kumbe wewe muuaji!? 
Jamaa:Ah,si kuna mzee nilitaka kumposa mwanae akanikatalia,mimi nikamuulia mbali. 
Mzee:Karibu baba, unataka harusi lini? Mimi sina tabu, Mkeo huyooo.!

Monday, September 10, 2012

Vijana na mahusiano...

Na Ikunda Faustine, Dar...


Nilikuwa namsikiliza Bi Ponza juzi anasema wasichana wa sasa hawajui kupika kabisa.Wengi wanaendekeza urembo sanaaa, vi-picha picha, vi-facebook nk. lakini kupika hawajui, Je ni kweli?

Nimekuwa nikisikia ili umkamate mwanaume pamoja na mautundu mengine uwe unajua kumpikia mahanjumati.Hivi ni kweli katika maisha tuliyopo wanaume wanajali sana kuhusu mapishi au mwanamke anaempikia madikodiko? TAFAKARI...

KWA WANAUME NAO:- MAMBO 6 WANAUME WASIYOYAPENDA  KUTOKA WA WENZA WAO.

1. Wanaume hawapendi kuambiwa cha kufanya na wenzi wao

Mwanamke unapotaka mwanaume afanye jambo usimwambie alifanye bali fanya kama una mpa ushauri.Kwamba John hivi kwa nini tusiweke balbu hapa kwenye korido maana kuna giza kweli usiku. Badala ya hivi "wewe John huoni hapa kwenye korido kuna giza balbu imeungua mwezi sasa hujabadilisha kwa nini? Weka balbu bwana". Atafanya au asifanye kabisa kwa sababu umemwambia cha kufanya tena kwa hasira.

2. Wanaume hawapendi mwenzi mwenye makelele, mlalamishi

Yeye ni kulalamika kuanzia jumatatu hadi jumapili. Japo wanawake nao wanasema kuna wanaume walalamishii balaaa. Na wenye gubu wanasusa kula mpaka kuongea wanawanunia wake zao mmmmh!

3. Wanaume hawapendi mwenzi mchafu

Mchafu wa mwili wake na hata nyumbani kwenye suala la kutunza nyumba wanayoishi. Uchafu hufanya mwanamke apoteze mvuto.

4. Wanaume hawapendi mwenzi mbishi

Japo na wanawake wanasema wanaume ndio wabishi zaidi. Utampa mwanaume  ushauri lakini haufanyii kazi ubishi mwingi mpaka kwenye mambo ya msingi.

5. Wanaume hawapendi kuamrishwa na mwenzi wao

Mwenzi mbabe anaetoa amri na  kumtawala hawataki.

6. Wanaume hawapendi kuhisiwa hisiwa na kusachiwa sachiwa

Kumpekua kwenye simu, mifuko ya suruali kwamba unamulika mwizi. Hawapendi, tena pengine hawajafanya jambo la kuwafanya wahisiwe vibaya.




Sunday, September 2, 2012

R.I.P Daddy...

Born 3rd March 1944 - Died 2nd September 1994

Saturday, September 1, 2012

Rest in Peace Meles Zenawi, Son of Africa.

Born : May 8, 1955 - Died : August 20, 2012
for more details of The Late Meles Zenawi CLICK HERE.