Popular Posts

Monday, February 13, 2012

Thamani ya Mapenzi Kushuka TZ - Nani wa Kumlaumu?


Tanzania ya leo ni tofauti kabisa na Tanzania ya miaka ya nyuma, hasa kwa Dar-es-salaam. Mwanamke kulala na mwanaume imekuwa ni kitu cha kawaida sana, sio kama zamani. Zamani mwanamke kulala nae sio kazi ndogo. Utaambiwa subiri nikafikirie, jibu wiki ijayoooooo! Pengine tungesema tatizo kwa sasa ni low self esteem na low self confidence kwa kina dada, lakini hata huko vyuoni nako ambako tunategemea kina dada zetu wasomi wawe tofauti, wao ndio wamepitiliza kabisa. Hao ndio wanao ongoza kwa mambo yote ya aibu mjini DSM. Makazini ndio usiseme, ni kawaida kwenda chooni na kusikia mke wa mtu anapiga mayowe ya mahaba. Kwa kweli tofauti na zamani, suala la sex halina thamani tena. Kwenye ndoa ndio kabisa, ni jambo la kawaida kwa wake za watu kulala na vidume vyao vya zamani, hata kama huko walipoolewa kuna kila juhudi za kuwaridhisha. Swali langu ni je, hali hii ya ngono ya ovyo ovyo na rahisi rahisi ni nani wa kulaumiwa zaidi kati ya wanaume na wanawake? Kwani humu kumekuwa na thread nyingi sana za kulaumu wanawake hawajatulia, mara nyingine wanaume hawajatulia, lakini huwa hakuna mjadala wa kusaidiana kupata majibu kuhusu chanzo la tatizo hili, hasa kwa kuzingatia kwamba huko nyuma hali haikuwa hivi.

No comments: