Popular Posts

Tuesday, February 7, 2012

Hoja ya Haja: Kwanini Wanaume Wengine Ni Waoga Wa Kutongozwa?"


Na Ikunda F. DSM.
Tusaidie. Baadhi ya wanaume ni waoga wa kutongozwa na wanawake. Hii ni kwa mujibu wa tafiti na uzoefu uliopo. Hapa kuna sababu za kijamii ikiwamo malezi, mila na desturi.
Bado inaonekana na wengi kama kitendo cha ajabu kwa mwanamke kuanza kuchukua hatua za kumtongoza mwanamme anayempenda ama kuvutiwa naye.
 
Kuna wanaume wanaoamini, kuwa jambo hilo si la ki-uanauke. Mwanamme bado anaamini kuwa jukumu la kuchukua hatua za kutongoza ni za kwake,kwamba ni yeye ndiye anayepaswa kuanza kumtongoza mwanammke. Akitongozwa anashtuka!
Inakuwaje basi,kama mwanamke atampenda ama kuvutiwa na mwanamme bila mwanamme huyo kuweza kusoma ishara za mapenzi, je, mwanamke huyo asubiri mpaka siku ile mwanamme atakapolala na kuota kuwa anapendwa na mwanamke huyo? Kazi kwako na wengine mlio tayari kuchangia. Tunasubiri maoni...

No comments: