Tafadhalini sikieni hiki kisa!!!!!!!!!!
Mama alikuwa na watoto watatu na hana MUME (single parent). Mtoto wa kwanza ni wa kiume na ana baba yake, wadogo wawili ni wa kike na wana baba yao. Mama kawasomesha watoto wake vizuri kwani wote wana shahada za uzamili (Master Degrees) ktk fani tofauti-tofauti.
Kaka alioa mdada BONGO FLAVOUR na mapenzi yao yalikuwa mazuri sana hadi pale walipogombana na mke kuamua kumkashfu (labda kumweleza ukweli), kashfa aliyodhani kuwa itamuumiza mwenzake hadi kumoyo na maini. Mke alimwambia mume "tatizzo la watu ambao hawakulelewa na kina BABA wanaoelewa hawajui mapenzi kabisa, hata uwafanyie nini hawawezi ku-appriciate.
Mume kusikia hivyo aliamua kutofanya lolote zaidi ya;
-Kumuachia gari la kuendea kazini ya yeye kuanza kupanda dalala.
-Kula chakula nje ya nyumba yao ingawa nyumbani wanapika
-Hela ya chakula na matumizi ya nyumbani inaachwa kama kawaida
-Hakuna maongezi wa mama yake maongezi
-Wanalala kitanda kimoja lakini hakuna mawasiliano yeyote
-Mke haruhusiwi kumfanyia mume vitu ambavyo katika hali ya kawaida anatakiwa kuwa anamfanyia kama kufua na kupiga pasi. Mume alikuwa akifanya mwenyewe au kwa dobi na vitu kama hivyo.
Mke alianza kupungua kwa mawazo na kujaribu kumrai mume wake amsamehe lakini mume alikuwa mara zote akigoma. Mambo yalipochacha mke alijifunga kibwebwe na kumvaa mama-mkwe na kumuelezea kila kitu. Bahati mbaya mamamkwe naye akija juu kwa kutukanwa kuwa ni malaya na hivyo kumfukuza na kutomsaidia mkamwana wake.
Mke aliamua kufunga safari kwenda Dodoma kwa Mjomba mtu aliyekuwa anasimama kama Baba na alimuaga mume wake na kupatiwa nauli ya kwenda huko. Ashukuriwe Mungu kwani Mjomba alikuw mwelewa na kukubali kumsaidia mkamwana wake. Mjomba aliongea na dadaye na kuyaweka sawa kabla ya kumvaa mume mtu.
Wanandoa hao kwasasa amani imerejea ktk nyumba. Tatizo ni kuwa haijulikani kama kweli amani hiyo ina upendo ule wa awali. UPENDO ILHALI WEWE NI MWANAHARAMU?
NB: Hamna kitu kibaya ktk ndoa kama kashfa; bahati mbaya dada zetu sababu ya kujua kuongea kuliko waume zao wamekuwa na kauli chafu na bila kuzifanyia kwanza uchambuzi kujua athari zake.
No comments:
Post a Comment