Popular Posts

Monday, August 9, 2010

Hii kitu haina urafiki..!!!


Kama kufuli la kichwani limeshindikana hayo mengine ni bure tu!!!! Soma hii...


Juma alimua kusafiri kwenda mbali. Akamvika mkewe chupi ya chumyenyea  kufuli. Ufunguo wa chupi alimwachia rafiki yake mkubwa na kipenzi kwa maelezo kuwa asiporudi baada ya miaka minne amfungulie mkewe ili aishi maisha ya kawaida.

Juma alianza safari yake. Muda si mrefu kabla hajafika mbali akamwona rafiki
yake kipenzi anamkimbilia…. akasimama kumsubiri kujua kulikoni.

Akauliza: Vipi rafiki yangu? Rafiki akajibu; umenipa ufunguo ambao si wenyewe!!!


Swali:- Amejuaje kama sio ufunguo wenyewe??? Inamaana alijaribu mapema sana, hata jamaa hajafika mbali! Na hakuona aibu kumwita na kuhiaji ufunguo wenyewe!!! kuna urafiki kwenye hii kitu kweli???

No comments: