Popular Posts

Wednesday, July 28, 2010

Ni Robo Tu Ya Wanaume Wa Dar Wenye Mbegu Zenye Rutuba

IMEFAHAMIKA, kuwa idadi ya wanaume wa Kitanzania wenye mbegu za uzazi
zisizorutubisha hivyo kutoweza kurutubisha yai la mwanamke na kusababisha mimba inaongezeka. Kwa mujibu wa gazeti la ‘ The Citizen’ toleo la Jumamosi ( Leo), Julai 17,2010 zaidi ya asilimia 35 ya wanaume wanaofanya vipimo vya rutuba za mbegu za uzazi wamegundulika kuwa hawana.

Mara nyingi lawama za kukosa mtoto katika familia zimekuwa zikielekezwa kwa
mwanammke kutokana na wanaume wengi kutokuwa na ujasiri wa kujitokeza kupima rutuba zao. Mazingira ya kazi, Mtindo wa maisha na hata hata kukaa kwa muda mrefu kwenye chumba chenye mvuke ni baadhi ya sababu zinazochangia wanaume kupungikwa rutuba za mbegu za uzazi.

Katika jiji la Dar es Salaam pekee, inaaminika kuwa ni asilimia 24.9 tu ya
wanaume wa Dar es Salaam walio na mbegu za uzazi zenye rutuba, hivyo, wenye
uwezo wa kurutubisha yai la mwanamke na hivyo basi, mimba kutokea.
Utafiti huo umefanywa na Idara ya Jinikolojia ya Hospitali ya Taifa Ya
Muhimbili.

No comments: